YANGA WATANGAZA VITA

ZAINAB IDDY NA WINFRIDA MTOI

YANGA imetangaza vita kuelekea mchezo wao dhidi ya Singida United kesho, huku mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiweka wazi jinsi walivyokerwa na wapinzani wao hao kuwakamia walipokutana nao hivi karibuni, huku wakilegeza dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar.

Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa na Singida United katika michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Katika mchezo huo wa robo fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Namfua, Singida, Aprili mosi, mwaka huu, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na hivyo mshindi kupatikana kwa changamoto ya matuta na ndipo wenyeji walipotoka uwanjani na ushindi na kutinga nusu fainali.

Lakini kabla ya kukutana na Yanga, Singida ilipokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, kabla ya wiki iliyopita kufungwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar, ukiwa ni mchezo wa ligi hiyo.

Na Yanga wanapokumbuka jinsi Singida United walivyowakamia walivyokutana Namfua, wanapatwa na hasira zaidi na hivyo kufikia uamuzi wa kutokuwa na mzaha na wapinzani wao hao wanaonolewa na kocha wao wa zamani, Hans van der Pluijm.

Wakizungumza na BINGWA jana, wachezaji wa Yanga walisema kuwa wamepania kuisambaratisha Singida United kesho ili kulipa kisasi cha kipigo cha mikwaju ya penalti walichokipata Namfua.

 

 

Inaendelea………….. Jipatie nakala ya Gazeti la #BINGWA

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*