WRIGHT: RAMSEY NENDA MAN U, SI CHELSEA

LONDON, England


MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal, Ian Wright, amemshauri kiungo wa timu hiyo, Aaron Ramsey ambaye mwishoni mwa msimu huu ataondoka ndani ya kikosi hicho bure.

Wright anafahamu kuwa kiungo huyo raia wa Wales anatakiwa na Chelsea, lakini amemwambia kuwa asitegemee mambo yatamwendea kiurahisi kama atajiunga na timu hiyo.

Hivi karibuni timu za Manchester United, Chelsea na Liverpool zimeingia vitani kuwania saini ya kiungo huyo ambaye hatosaini mkataba mpya ndani ya Arsenal.

“Ramsey ni mchezaji mzuri sana, nasikitika hatakuwepo Arsenal msimu ujao, lakini namshauri asiende Chelsea sababu Ross Barkley na Ruben Loftus-Cheek watamweka benchi.

“Labda aifikirie Manchester United ambayo inasemekana Juan Mata ataondoka Januari,” alisema mkongwe huyo aliyewahi kuwa straika hatari enzi zake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*