googleAds

Wolper awang’ata sikio warembo

NA BRIGHITER MASAKI

MWIGIZAJI na mbunifu wa mavazi Bongo, Jacqueline Wolper, amesema kama kigezo cha kuolewa kingekuwa sura, basi yeye angekuwa tayari ameolewa.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Wolper alisema warembo wengi huwa wanajidanganya kuwa uzuri ni sura lakini wanasahau tabia.

“Unakuta msichana mrembo sana lakini haolewi kwasababu hana sifa za kuwa mke wa mtu kwa hiyo wasichana warembo wajikague tena,” alisema Wolper.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*