WASANII WAKONGWE WABADILISHE AINA YA MUZIKI SI KUACHANA NAO


WASANII wakongwe katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, wamekuwa wakitangaza kujiweka pembeni na sanaa hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kukataliwa na kutokupokewa vizuri kazi zao.

Kwa sasa muziki umekuwa mgumu kutokana na wadau kushindwa kuwapa sapoti kama ilivyokuwa awali na badala yake wasanii wapya ndio wanaokuja juu na kutengeneza fedha kutokana na muziki kuuza.

Suala hilo linatoa ishara kuwa muziki umebadilika na unahitaji umakini pamoja na nidhamu ya juu ili kuweza kuendelea kudumu hasa kipindi hiki ambacho damu changa zinaonekana kupendwa zaidi.

Mijadala mingi imeibuka kutokana na hatua hizo za wasanii wakongwe katika muziki kuamua kujiweka pembeni bila kutambua kuwa muziki si kandanda kusema kuna muda wa kustaafu.

Kinachofanya wasanii hao waone muziki umewatupa, ni kutumia mbinu na mikakati ya zamani wakitarajia kupata matokeo tofauti.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*