Wasanii Uzalendo Kwanza waonyeshwa viwanja vyao

NA BRIGHITER MASAKI

KAMPUNI ya KC Land Development Plan imewapeleka wasanii wanaounda Chama cha Uzalendo Kwanza katika viwanja watakavyopewa vilivyopo eneo la Mwasonga, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la Burudani juzi, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere, alisema anaishukuru kampuni hiyo kwa kuwafikiria wasanii na watu masikini katika kuwawezesha kwenye suala la kumiliki ardhi.

“Wasanii tumekuwa tukitangatanga katika nyumba za kupanga, tunawashukuru KC kwa kutuona na kutuwezesha kupata ardhi kwani wangeweza kuwauzia matajiri lakini mmetufikiria sisi wasanii tunashukuru na tunawaahidi kuwa hatutauza viwanja bali tutajenga mtaa utakuwa ni wetu wasanii,” alisema Steve.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya KC,  Halid Mwinyi, alisema: “Tumejipanga kuwakwamua wananchi wa chini, tumeanza na wasanii baada ya hapo tutafuata makundi mengine kwa mkopo usiokuwa na riba, viwanja tumewaonyesha hapa Kigamboni japo kuna maeneo tofauti Mkoa wa Pwani pamoja na Dodoma, kama mnavyoona tunaendelea kuweka barabara na hospitali na umeme,” alisema Mwinyi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*