googleAds

WARUSI WAZIDI KUSOMBA MEDALI OLIMPIKI

BUENOS AIRES, Argentina

TIMU ya Taifa ya Urusi imeendelea kujizolea medali katika michuano ya Olimpiki ya vijana yanayoendelea mjini Bueno Aires, nchini Argentina, baada ya mwogeleaji wake mwingine, Andrei Minakov, kufanikiwa kutwaa nyingine ya dhahabu ya kuogelea upande wa wanaume umbali wa mita  100 mtindo wa butterfly.

Staa huyo alitwaa medali hiyo juzi, baada ya kutumia muda wa sekunde 51.12, akifuatiwa na raia mwingine wa nchi hiyo, Kristof Milak, ambaye alitumia muda wa sekunde 51.50.

Katika mbio hizo, nafasi ya tatu ilikwenda kwa Muitaliano, Federico Burdisso, ambaye alitumia muda wa sekunde 52.42.

Tayari timu ya Taifa ya Urusi imeshanyakua medali 16 katika mashindano ambapo kati ya hizo, 13 ni za dhahabu, mbili za fedha na moja ikiwa ni ya shaba.

Timu hiyo inafuatiwa na Hungary, yenye jumla ya medali 9 saba, zikiwa ni dhahabu moja ya fedha na moja ya shaba, ikifuatiwa na Italia, ambayo ina medali 11, mbili za dhahabu, nne za fedha na tano za shaba.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 18, mwaka huu.

 

 

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*