Wakongwe wamshukia Rashford, kisa kiwango chake

MAMBO si shwari klabuni Manchester United huku presha ikitanda kwa kocha anayeinoa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer, kwa kile kinachoendelea.

Kikubwa ni kiwango kisichoridhisha kinachoonyeshwa na mshambuliaji wao tegemeo, Marcus Rashford.

Wachezaji wakongwe waliowahi kutamba miaka ya nyuma akiwamo Alan Shearer na Martin Keown, hata hivyo wamemtetea na kusema pengine kikosi kizima cha Man United kimesababisha uwezo wa Rashford kushuka.

Rashford mwenye umri wa miaka 21 inapitia katika wakati mgumu kwenye kikosi hicho huku akiwa na hofu ya kupoteza namba kwenye timu ya taifa ya England.

Shearer aliyewahi kutamba akiwa na Southampton, Blackburn Rovers na Newcastle, amesema mshambuliaji huyo hapati huduma anayostahili ya kucheka na nyavu anapokuwa eneo la hatari.

“Hiki ni kikosi kibovu cha Man United kuwahi kutokea, pengine hii ni sababu kubwa ya Rashford kuonekana ancheza ovyo,” alisema Shearer. Naye kwa upande wake, Keown ana imani Rashford hapati ushirikiano kutoka kwa viungo wake.

“Rashford ni mchezaji mzuri nadhani tatizo ni wale wanaomzunguka kutompa huduma anayostahili,” alisema Keown.

Man United imeendelea kukumbwa na lundo la majeruhi akiwamo Jesse Lingard, Anthony Martial, Aaron Wan- Bissaka, Paul Pogba, Victor Londelof na Luke Shaw ambao huenda wakaukosa mchezo unaofuata dhidi ya Liverpool.

Man United imepoteza mechi zake tatu mfululizo za Ligi Kuu England na inashika nafasi ya 12 baada ya kujikusanyia pointi tisa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*