WAKALI WAO WAZIPIGA BAO JAHAZI, MASHAUZI CLASSIC

KUNDI la Wakali Wao linalosimamiwa na Tabit Abdul, limezipiga bao bendi za Jahazi na Mashauzi Classic kwa kumrudisha mwimbaji wao, Asya Mariam ‘Utamu’. Utamu aliyekuwa akiwaniwa na bendi hizo maarufu nchini zenye upinzani mkubwa, ameamua kurejea kwenye bendi yake ya zamani ya wakali wao Akizungumza na gazeti hili, Mariam alisema amerejea rasmi kwenye bendi hiyo baada ya kutofautiana na uongozi wake chini ya Tabit Abdul. “Hata vikombe kabatini hugongana ndiyo maana mimi nikawa na tatizo na uongozi wangu nashukuru nimeweza kumaliza matatizo yangu na nimerejea rasmi,” alisema. Alisema kwa sasa atakuwa akionekana kwenye majukwaa ya bendi hiyo kama kawaida na kuwataka mashabiki wake wajiandae kupata burudani Awali Mariam alikuwa haonekani kwenye majukwaa ya kundi hilo kutokana na kutofautiana na uongozi wake lakini sasa wamemaliza tofauti zao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*