Wadau soka waamke kuzisaidia Mtibwa Sugar, Biashara United

Wadau soka waamke kuzisaidia Mtibwa Sugar, Biashara United

TIMU ya Mtibwa Sugar imeendelea kufanya vibaya Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kufungwa michezo mitatu mfululizo.

Msimu huu unaonekana ni mbaya kwa timu hiyo, tofauti na miaka mingine iliyokuwa inaanza vizuri, licha ya kushindwa kumaliza katika nafasi mbili za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Tangu Ligi Kuu ilipoanza Septemba 23, mwaka huu, Mtibwa Sugar imeshafungwa mabao 3-1 na Lipuli, wakapoteza mchezo mwingine kwa kuchapwa mabao 2-1 na Simba, kisha kupata sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania, kabla ya kufungwa mabao 3-1 na Tanzania Prisons.

BINGWA haturidhishwi na mwenendo wa Mtibwa Sugar na timu nyingine , ikizingatiwa kuwa ni moja kati ya timu zilizotarajiwa kuonesha kiwango kizuri ili kuifanya ligi kuwa ya ushindani.

Kwa upande wetu, tunaona ni tatizo ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar, kama ilivyo kwa timu ya Biashara United ambayo pia haiko katika ushindani wa soka kutokana na kupoteza baadhi ya michezo yao.

Kuendelea kufanya vibaya kwa timu ya Mtibwa Sugar na Biashara United, pengine kunachangiwa na mambo mengi ambayo yanaweza kutatuliwa iwapo yatawekwa wazi na wadau wa mikoa hiyo kuyasikia na kuyafanyia kazi.

Tunaamini timu hizo zinaweza kufanya vizuri michezo inayofuata ikiwa zitakuwa zimebaini chanzo cha tatizo la kutopata matokeo mazuri katika michezo iliyochezwa hadi sasa.

BINGWA tunaamini mwanzo mbaya kwa Mtibwa Sugar, Biashara United na timui zingine unaweze kuwa mzuri baadaye ikiwa wadau wa mikoa zinakotoka timu hizo wataamka kuzisaidia kabla ya jahazi kuzama.

Tunasema hivyo tukijua kwamba timu hizo ndizo zinazoibeba mikoa yao katika  soka, ikizingatia baadhi ya mikoa hazina timu za Ligi Kuu Bara kwa miaka mingi.

Itakuwa vema endapo wadau wa soka wa mikoa wataona umuhimu wa kuwapo karibu na viongozi, wachezaji na mabenchi ya ufundi ili kutibu tatizo lililozikumba timu zao kabla ya kupoteza kabisa mwelekeo katika ligi hiyo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*