Wachezaji kikapu watakiwa kujipanga kwa ligi

NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF), umewataka wachezaji wanaotarajia kucheza ligi mbalimbali kuendelea na mazoezi yao binafsi ili kujiweka tayari kushiriki ligi zao.

Kwa sasa Serikali imepiga marufuku mikusanyiko ya watu, ikiwamo michezo kutokana na kusambaa kwa virus vya corona ambavyo vimechangia maelfu ya vifo vya watu duniani.

Akizungumza na BINGWA jana, Rais wa TBF, Phares Magesa, alisema kutakuwa na ligi za mikoa ambazo ni muhimu zenye kupata timu zitakazoshiriki katika Ligi ya Taifa ya mchezo huo.

Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha ligi zitakapoanza katika mikoa ziwe na ushindani mkubwa kwa timu  zitakazoshiriki.

“Tunatoa msisitizo kwa wachezaji kufanya mazoezi yao binafsi kwa kujituma kwa bidii ili kutoa nafasi kwa makocha kufanya marekebisho madogo madogo kwa pamoja,” alisema Magesa. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*