Wabaguzi wamtibua nyongo Balotelli

MILAN, Italia

IMEKUWA ni wikiendi ngumu kwa Mario Balotelli na timu yake Brescia, kwanza akishuhudia wakipokea kichapo cha mabao 2-1 huku nay eye akibaguliwa na mashabiki wa Verona.

Katika mchezo huo uliochezwa wikiendi iliyopita, Balotelli aliweza kufunga bao la kufutia machozi, lakini alikutana na wakati mgumu kutokana na mashabiki hao kumtolea maneno yaliyoashiria ubaguzi kabla ya kuwabutulia mpira kwa hasira.

Kama hiyo haitoshi, Balotelli alitishia kutoka uwanjani kabla ya wachezaji wenzake na wale wa Verona kumtuliza hasira zake na aliweza kuendelea na mchezo huo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*