googleAds

Waamuzi watakiwa kubukua upya sheria za soka

NA ZAINAB IDDY

MWENYEKITI wa Kamati ya Waamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Soud Abdi, amesema waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili, wanatakiwa kujikumbusha kusoma sheria 17 za soka.

Soud alisema lengo la kufanya hivyo ni kuzifahamu sheria kwa ufasaha zaidi ili kuondoa uamuzi wa utata.

Abdi alikabidhiwa majukumu ya kamati hiyo Februari 20, mwaka huu, baada ya TFF kufanya mabadiliko katika kamati zake ndogo ndogo.

Alisema kumekuwa na uamuzi wa ovyo unaofanywa na waamuzi wanaochezesha ligi, jambo linalochangia kupatikana kwa matokeo yenye utata.

“Mapumziko ya siku 30 yanatosha sana kwa mwamuzi mwenye nia ya dhati ya kufanya kazi yake kwa uweledi kujifunza au kujikumbusha kanuni mbalimbali za soka.

“Natamani kuona ligi zitakaporejea kila mwamuzi afanye kazi yake kwa kufuata misingi ya sheria zilizowekwa, kupitia upya sheria ili kuongeza uelewa na kutawasaidia sana.

“Mfano hili tatizo la ‘off side’ (kuotea), limeonekana ni janga kubwa na limesababishwa na kubadilika kwa sheria za soka, hivyo kama kila mwamuzi akijikumbushia kusoma jambo moja, hadi siku 30 zikimalizika, atakuwa ameelewa vingi,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*