googleAds

VIPIGO BARCA, MADRID VYAWEKA REKODI

MADRID, Hispania


 

REAL Madrid imeshindwa kutumia faida ya Barcelona kupewa kichapo cha aibu dhidi ya Leganes, na timu zote hizo zimeweka rekodi ya kufungwa ndani ya siku moja, kwa mara ya kwanza tangu Januari, 2015.

Mabingwa watetezi wa LaLiga na vinara wa ligi hiyo, Barca, walikubali kipigo cha mabao 2-1, huku bao la ushindi likifungwa na mchezaji wa Madrid aliyeko Leganes kwa mkopo, Oscar Rodriguez.

Madrid walikuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi juzi, lakini walijikuta wakipigwa na Sevilla katika mechi ya kwanza ya ligi chini ya kocha wao mpya, Julen Lopetegui.

Mabao mawili ya straika Mreno, Andre Silva na moja la Wissam Ben Yedder, yalitosha kuwaliza Madrid, na vichapo hivyo vilikuwa ni taarifa nzuri mno kwa Atletico Madrid, ambao wapo nafasi ya tatu, kwa tofauti ya pointi mbili.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*