googleAds

Verrati ampiga ‘stop’ Neymar

PARIS, Ufaransa

KIUNGO wa PSG, Marco Verratti, amemtaka Neymar, kuachana na mpango wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo.

Akizungumza baada ya mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Ufaransa, maarufu Ligue 1 dhidi ya Nimes, kiungo huyo alisema Neymar ni mchezaji muhimu katika kikosi chao.

“Neymar ni rafiki yangu wa karibu, amefanya makubwa PSG, amefunga mabao mengi na muhimu msimu uliopita, hivyo nitaumia endapo ataondoka,” alisema Verrati.

Neymar aliukosa mchezo huo ambao PSG iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao hao.

Awali, nyota huyo alitajwa na vyombo habari kuwa yupo mbioni kurejera Barcelona, baada ya kuishawishi PSG kumwachia.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*