Vanessa Mdee na prodyuza wa Beyonce wafanya jambo

CALIFORNIA, MAREKANI

MREMBO anayeendelea kufanya vyema kwenye Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, ameingia studio kufanya kazi na mtayarishaji maarufu wa muziki duniani, Nick Cooper, anayefanya kazi na mastaa kama Beyonce, Nick Minaj na J Lo huko California, Marekani.

Vee Money ambaye yupo kwenye ziara yake ya kimuziki nchini humo, juzi aliwajuza mashabiki zake kuwa amefanikiwa kuingia kwenye studio hizo kufanya nyimbo zitakazokuwa kwenye albamu yake ya pili.

“Nimebahatika kuingia studio na ‘vocal producer’ maarufu duniani Nick Cooper ambaye anafanya sauti za kina Beyonce, Nicki Minaj, J Lo, naomba niseme albamu yangu ya pili itakuwa moto tayari imekamilika asilimia 70,” alisema Vanessa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*