Vanessa Mdee, Lil Ommy wapamba jarida kubwa Nigeria

NA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na mtangazaji nyota Bongo, Omary Tambwe ‘Lil Ommy’, wamepamba toleo la 23 la jarida kubwa la Tush Magazine, linaloangazia vijana wenye mafanikio kwenye sekta za burudani Afrika.

Vanessa alipamba ukurasa wa mbele wa Tush Magazine huku sababu kubwa ikiwa ni historia yake ya muziki kutoka alivyoanza mpaka alivyopata mafanikio, huku Lil Ommy (King Of Interviews, The MVP) naye akipamba ukurasa wa ndani kwa makala inayoelezea mafanikio aliyonayo sasa kwenye utangazaji wa vipindi vya burudani.

Jarida hilo lenye mrengo wa vijana, limesheheni habari, mahojiano na makala za mastaa mbalimbali katika tasnia za muziki, mitindo, filamu, teknolojia, matamasha, mahusiano na biashara.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*