googleAds

VAN VICKER ATUA BONGO KUMSAPOTI WEMA

NA JEREMIA ERNEST


 

MWIGIZAJI nyota wa kimataifa kutoka Ghana, Van Vicker, amewasili nchini jana tayari kushiriki sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Wema Sepetu, itakayoambatana na uzinduzi wa filamu yao, Day After Death (D.A.D) katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la Burudani alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Van Vicker, alisema anajivunia kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kwani licha ya kutokuwapo kwa Steven Kanumba, kuna wasanii wenye uwezo.

“Ni fahari kwangu kufanya kazi na wasanii wa Tanzania, imekuwa ikinijenga katika sanaa kwa kuwa wanajua huu ni mwanzo tutegemee filamu nyingine nitakayocheza na Wema kwa mara ya pili,” alisema Van Vicker.

Aliongeza kuwa mbali na Wema Sepetu, anatamani kufanya kazi na mwigizaji mkongwe, Mzee Hashim Kambi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*