googleAds

Uwoya, Barnaba kuipamba Miss Moro

MICHAEL MAURUS, MOROGORO

MSANII mahiri wa filamu, Irene Uwoya na mkali wa Bongo Fleva, Barnaba, wanatarajiwa kupamba kinyang’anyiro cha Miss Morogoro 2019, kwenye ukumbi wa Morogoro Hoteli, mjini hapa leo, huku kukiwa na shoo kali kutoka kwa mkali wa muziki wa dansi, Christian Bella.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Farida Kulususu, jumla ya warembo 12 watapanda jukwaani kuwania taji hilo, ikiwa ni mchakato wa kuelekea kumpata Miss Tanzania 2019, kuwania taji linaloshikiliwa na Queenelizabeti Makune.

Farida alisema kuwa warembo hao walikuwa wakifuliwa vilivyo katika ukumbi wa Nyumbani Park, maarufu kama Samaki Samaki, mjini hapa, akiwaahidi wadau wa urembo na burudani bonge la shoo. “Itakuwa ni shoo ya aina yake, tuna warembo wazuri mno na wamepikwa vilivyo, hivyo wadau wa urembo na burudani kwa ujumla waje kwa wingi, ukizingatia tutakuwa na mkali wa dansi, Christan Bella atakayetoa shoo kabambe,” alisema Farida.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*