googleAds

Usajili Simba wamuibua Niyonzima

NA GLORY MLAY

KIUNGO wa zamani wa Simba, Haruna Niyonzima,  amesema  hakuna timu itakayowazuia Wekundu wa Msimbazi kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza na BINGWA jana, Niyonzima alisema kutokana na usajili wao uliosheheni wachezaji nyota, wanaweza kuchukua ubingwa mapema kabla ya kufikia mzunguko wa mwisho wa ligi ijayo. 

Niyonzima alisema  ukilinganisha na timu nyingine ambazo zinajiandaa na  Ligi Kuu msimu ujao, utaona Simba wamefanya usajili mzuri.

Alisema wachezaji wanaonekana kuwa ni wazuri wakishirikiana watani wao wa jadi Yanga wasahau kuchukua ubingwa wa msimu ujao.

“Ndiyo, Simba wamefanya usajili wa maana na wana wachezaji wenye uwezo ukilinganisha na timu nyingine, japo zinajitahidi kusajili wachezaji mbalimbali kutoka nje,” alisema Niyonzima. 

Katika usajili wa msimu ujao, Simba imewasajili, Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Viera na Wilker Henrique da Silva.

Wengine ni Francis Kahata, Deo Kanda, Sharaf Shiboub, Ibrahim Ajib, Gadiel Michael, Beno Kakolanya, Miraji Athuman na Kenedy Juma.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*