UMESIKIA HII YA SHABIKI NA OZIL?

London, England

KIUNGO wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, amemshukuru shabiki wa timu yake hiyo aliyeonesha kuwa anamkubali Mjerumani huyo hadi kufikia uamuzi wa kumpa mwanaye wa kiume jina la Mehd Ozil.

Baba wa mtoto huyo, Inzamam-Ul-Haq na mkewe, walipata mtoto huyo wa kiume Desemba mwaka jana, lakini kabla hajazaliwa, tayari baba alishaamua mwanaye ataitwaje.

“Marafiki na familia yangu wananijua. Kila ninachokifanya lazima kihusiane na Arsenal,” alifafanua Inzamam kwanini alimuita mwanaye jina hilo.

Ozil aliposikia habari hiyo, alimshukuru baba huyo na kutania kwamba, Mehd Ozil ataisaidia familia yake kwa mambo mengi.

Ozil aliandika kwenye Twitter:     “Nafarijika kuona mtoto akipewa jina langu. Niwatakie maisha mema huko India. Naamini ataisaidia mno familia yake.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*