googleAds

UMESIKIA ALICHOKISEMA DANNY STURRIDGE?

LONDON, England


SIKU chache baada ya Eden Hazard kudai bao alilowafunga Liverpool kwenye Kombe la Carabao, ni moja ya mabao bora aliyowahi kuyafunga, Daniel Sturridge naye amejibu mapigo.

Wikiendi iliyopita kulikuwa na mechi kali ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea na Liverpool, mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1, kwa mabao yaliyofungwa na Hazard na Sturridge.

Sturridge alifunga bao hilo kwa shuti kali la umbali wa yadi 30 na kuipa timu yake ya Liverpool pointi moja muhimu.

“Ni bao kubwa sana kwangu na kwa Liverpoool. Nadhani nimefunga mabao mengi mazuri, ila hili ndilo lenyewe,” alisema Sturridge.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*