googleAds

Umemsikia Wijnaldum wa Liver?

MERSEYSIDE, England

STAA mpya wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, ni kama amewatisha mashabiki wa timu pinzani, akiwaambia kocha wake, Jurgen Klopp, anajipanga kufanya mambo makubwa klabuni hapo.

“Ni kikosi chenye vipaji na kocha bora,” alisema Wijnaldum na kuongeza: “Naamini kuna kitu anajaribu kukijenga. Nilihisi hivyo siku ya kwanza kukutana na Jurgen Klopp.”

Kiungo huyo raia wa Uholanzi, alitua Anfield siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili akitokea Newcastle United.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*