UKISIKIA KISA CHA BEKI WOLVES UTACHEKA

LONDON, England


AMA kweli majuu hamnazo. Beki wa timu ya Wolverhampton inayoshiriki Ligi Kuu England, Ryan Bennett, amekasirishwa mno na kitendo cha wezi kung’oa matairi ya gari lake la kifahari aina ya BMW.

Bennett alitoa taarifa hiyo katika mtandao wa kijamii wa Twitter asubuhi ya jana, akiomba msaada wa kuwatafuta wezi hao waliofanya kitendo hicho usiku wa kuamkia jana.

“Aisee! Nimeamka asubuhi tu nimekuta gari langu halina matairi. Yeyote aliyeuziwa matairi aina ya Dunlop tafadhali anijulishe!” aliandika Bennett katika ‘posti’ yake hiyo.

Beki huyo ameitumikia timu yake hiyo mpya msimu huu ya Wolves katika mechi zote nne za Ligi Kuu na ameisaidia kukusanya pointi tano.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*