Uganda wagoma kisa posho

CAIRO, Misri

TIMU ya taifa ya Uganda, imegoma kufanya mazoezi baada ya kutolipwa posho zao walizoahidiwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019), inayoendelea nchini Misri.

Ahadi hiyo walipewa kutokana na ushindi waliopata wa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo na sare walipocheza na Zimbabwe.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Uganda, fedha wanazodai ni pauni milioni 6,000 (Sh bil.4) kama bonasi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*