googleAds

TUUNGANISHE NGUVU KUIANDAA SERENGETI BOYS

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imepata nafasi ya kushiriki fainali za Vijana wa Afrika kwa umri huo baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Congo Brazzaville.

Uamuzi huo ambao umefikiwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) katika vikao vyake huko Gabon, umeipa nafasi hiyo Tanzania baada ya Congo kushindwa kumpeleka mchezaji aliyelalamikiwa na TFF kwamba alichezeshwa huku akiwa amezidi umri.

Zimebaki wiki sita tu kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yamepangwa kuanza Aprili 2, mwaka huu nchini Gabon. Lakini kwa muda uliobakia ni mdogo sana kwa maandalizi ya uhakika ya timu hiyo hasa kwa kuzingatia kwamba kambi ya timu hiyo ilivunjwa.

BINGWA tunawataka wadau wote wa mchezo wa soka hapa nchini kuunganisha nguvu kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania kuhakikisha timu hiyo inapata kambi nzuri na maandizli ya uhakika, japo muda ni mfupi ila ni vyema kuhakikisha timu hiyo inakwenda kuwa mshindani wa taji na si mshiriki kwenye mashindano hayo.

Kwa kutambua hali ya ugumu wa michuano hiyo na kundi ambalo timu yetu imepangwa, ni muhimu sana timu ikapata wasaa wa kujiandaa vyema huku TFF ikihakikisha kwamba bechi la ufundi la timu hiyo linarudi kama lilivyokuwa zamani badala ya kulibadilisha katika hatua hii.

BINGWA tunaimani kubwa na vijana wa Serengeti kutokana na uwezo walionao,  tunawatakia kila la heri katika maandalizi yao huku tukisisitiza umoja na mshikamo kama Taifa katika kuipa sapoti timu hiyo ya Vijana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*