TUKUTANE KWA ‘MCHINA’, HAPA KING KIBA, PALE SAMATTA

Lulu Ringo na Johns Njozi, Dar es Salaam          |           


Mtanzania anayesukuma kabumbu nchini Ubelgiji katika Timu KRC Genk, Mbwana Samatta na Msanii Ally Kiba, kesho watakamilisha kampeni yao ya ‘Nifuate’ kwa mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini dare s Salaam saa tisa alasiri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Juni 8, Msemaji wa Timu ya Samatta, Lucas Mhuvile maarufu Joti, ametangaza kiama kwa timu Kiba kujiandaa kwa kipigo.

Kwa upande wake, Samatta amesema lengo la mechi ya nifuate linajulikana ni kusaidia elimu lakini yeye na Ali Kiba wamepania kutoa burudani kwa Watanzania watakaofika uwanjani siku ya kesho.

“Pamoja na hayo lakini pia lengo ni kutengeneza ushirikiano baina ya vijana maarufu wa kitanzania waweze kulisaidia taifa katika mambo yenye maendeleo.

“Lengo la mechi hii si kukusanya hela, lengo ni kusaidia kwaiyo kitakachopatikana ndiyo tutakachokwenda kusaidia,” amesema Samatta.

Kampeni hiyo ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kuchangia mfuko wa elimu na vijana, walengwa wakiwa ni wanafunzi wa shule za msingi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*