TSHISHIMBI SAFI YANGA

NA MWAMVITA MTANDA


*Aliyemleta asema hakuna Yanga bila kiungo huyo, kubaki Jangwani kwa gharama yoyote

WAPENZI wa Yanga wamepewa habari njema juu ya kiungo wao mkabaji, Papy Tshishimbi, kuwa ataendelea kuwapo Jangwani kwa gharama yoyote ile.

Hivi karibuni kulienea habari za kiungo huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa yupo njiani kuondoka Yanga, huku akihusishwa na Simba na Azam.

Japo bado ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi, ilidaiwa kuwa, Simba na Azam walikuwa wakimpigia hesabu kumng’oa Jangwani, kutokana na kuvutiwa na kiwango chake.

Habari hizo zilionekana kuwaumiza mno mashabiki wa Yanga, hasa kutokana na kiwango alichokionyesha katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakiamini alikuwa ‘akiwaaga’.

Lakini wakati vuguvugu la usajili likiendelea kupamba moto, mashabiki, wapenzi na viongozi wa Yanga wamehakikishiwa kuendelea kufaidi uhondo wa mchezaji huyo msimu ujao.

Akizungumza na BINGWA juzi, Meneja wa Tshishimbi, Shaaban Hussein ‘(Ndama Mtoto wa Ng’ombe’), alisema kuwa kiungo huyo ataendelea kuwapo Yanga msimu ujao, hivyo wapenzi wa timu hiyo wasiwe na ‘mchecheto’……………

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA hapo juu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*