TORRES ‘KUVUNJA NDOA’ NA ATLETICO MADRID

MADRID, Hispania

STRAIKA wa Atletico Madrid, Fernando Torres, ametangaza kuwa ataondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mfumania nyavu huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea, amebakiza miezi michache kwenye mkataba wake na amepanga kutafuta timu atakayocheza mara kwa mara.

“Napenda kutumia fursa hii kutangaza kwamba huu utakuwa ni msimu wangu wa mwisho,” alisema Torres.

“Niliona huu ndio wakati wa kuwaweka wazi mashabiki wangu. Nadhani sina budi kukubaliana na ukweli kwamba umefika wakati niwaachie wengine nao waendeleze gurudumu,” aliongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*