Torres: Huu ni wakati mzuri wa kupambana na Barcelona

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres, ameweka wazi morali ya hali ya juu aliyonayo kwa kusema kuwa, wakati huu ndio mzuri kupambana na Barcelona kwenye mtanange wao wa La Liga wiki hii.

Torres aliiongoza Madrid kuinyuka klabu ya Sporting Gijon mabao 5-0, huku wapinzani wao watakaokutana nao mapema wiki hii, Barca wakiitandika Leganes mabao 5-1 wikiendi iliyopita.

“Barca ni wapinzani wetu wagumu, ni vizuri ukikutana nao kipindi unachokuwa na mwenendo mzuri,” alisema.

“Kiujumla tuna furaha kupata pointi tatu kwenye mchezo na timu ngumu kama Sporting, tulipania kupata ushindi na si  sare,” aliongeza Torres.

Atletico Madrid na Barca zinatarajiwa kuumana kwenye mtanange mkali wa La Liga utakaopigwa dimba la Camp Nou usiku wa Jumatano.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*