TIWA SAVAGE UMEMSIKIA WIZKID LAKINI?

LAGOS, Nigeria


HUKU Tiwa Savage akielezwa kunasa katika uhusiano wa kimapenzi na Wizkid, jamaa huyo ametamka wazi kuwa huwa hawezi kutulia na mwanamke mmoja.

Kwa nyakati tofauti, Wizkid ameshawahi kutoka na warembo Sola Ogudu, Binta Diallo na Jada Pollock, kila mmoja akimpatia mtoto wa kiume.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio hivi karibuni, staa huyo alisema anapenda ‘mademu’, hivyo hawezi kutulia na mmoja.

“Hiyo ni ngumu kwa sababu nina wanawake wengi ambao nawapenda kinoma” alisema.

Wizkid amejitosa kwa Tiwa Savage na mara kwa mara wamekuwa wakionekana pamoja, ikiwamo hivi karibuni walipojiachia kimahaba baada ya tamasha la Afrorepublik lililofanyika jijini London, Uingereza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*