TIGO FIESTA… MOTO KUWAKA MULEBA

NA MWANDISHI WETU


 

BAADA ya Tamasha la Tigo Fiesta kutofanyika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera mwaka jana, leo limerudi tena na shangwe lake linatarajiwa kuwa bab kubwa kwenye Uwanja wa David Zihimbile.

Kwa mara ya mwisho onyesho hilo kwa Wilaya ya Muleba lilifanyika mwaka 2016 kwenye uwanja huo wa David Zihimbile na wasanii mbalimbali kam Mr Blue, Maua Sama, ilikuwa zamu ya watu wa Muleba mkoani Kagera, kama hukubahatika kuwepo Muleba basi nakusogezea picha 15 ujionee Fiesta ilivyohappen mkoani hapo.

Wakali wa Bongo Fleva waliopanda stegini ni Maua Sama, Baraka da Prince, Manfongo, Jux, Msami, Darassa, Joh Makini, Shilole, Chegge, Christian Bella, Navy Kenzo na Sholo Mwamba.

Kama ilivyokuwa kwa onyesho hilo la Muleba kwa wasanii kukamua vilivyo ndivyo litakavyokuwa lile la leo, huku baadhi ya wasanii waliokamua mwaka juzi walikuwamo na leo watakuwapo pia.

Wasanii ambao mwaka juzi walitoa burudani kwenye onyesho hilo ambao watakuwapo leo ni Mau Sama, Chegge, Mr Blue, Stamina na Joh Makini.

Wasanii wengine watakaoshiriki kwenye onyesho hilo leo ni Roma Mkatoliki atakayeshirikiana na Stamina na kuunda kundi lao la Rostam, wengine ni Lulu Diva, Fid Q, Barnaba na wengine wengi.

Akizungumzia tamasha la Muleba, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner G. Habash, aliwahakikishia burudani ya hali ya juu wote watakaohudhuria tamasha hilo mjini humo.

“Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Mbali ya kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama ntilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,” alisema Habash.

Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga: “Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018, zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu Sh 5,000 pekee badala ya Sh 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslimu.

“Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.”

Mpinga aliongeza: “Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*