googleAds

TFF yazipiga mkwara klabu za FDL

NA GLORY MLAY

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) itakayoshindwa kulipa Sh. 315,000,  ikiwa ni ada na leseni ya wachezaji haitashiriki ligi hiyo, itakayoanza keshokutwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Mashindano wa TFF, Baraka  Kizuguto,  alisema kila klabu inatakiwa kulipa Sh. 300,000 ikiwa ni ada ya ushiriki na Sh. 15,000 kwa ajili ya leseni ya mchezaji.

Kizuguto alisema mchezaji  hataruhusiwa kucheza ligi hiyo bila kulipiwa leseni, kwani watakuwa wamevunja taratibu na sheria zilizowekwa.

“Timu zinatakiwa kufika ofisini kuanzia leo (jana) kuchukua leseni za wachezaji wao, hatutakuwa na huruma kumruhusu mchezaji kucheza ligi  bila leseni huo utakuwa ni ukiukwaji wa sheria,” alisema Kizuguto.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*