Tetema ya Rayvanny yatua Marekani

NA MWANDISHI WETU

WIMBO wa Tetema wa Rayvanny na Diamond Platnumz, umetua kwa kishindo Marekani mara baada ya rapa maarufu nchini humo, Kevin Gates, kuuweka kwenye orodha ya ngoma anazozisikiliza kwenye gari lake.

Gates mwenye asili ya Morocco, juzi aliweka video katika ukurasa wake wa Instagram mwenye mashabiki milioni 7.2, ikimwonyesha akiwa ndani ya gari lake na kuufurahia wimbo huo.

Rayvanny na Diamond Platnumz wameendelea kufurahia mafanikio ya Tetema ambao ulifikisha watazamaji milioni 2 ndani ya siku mbili, huku ukishika namba moja kwa kutazamwa zaidi Tanzania, Kenya na Uganda.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*