TBF wahaha kusaka wadhamini

NA GLORY MLAY

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), linaendelea kusaka wadhamini ili kufanikisha maandalizi ya michuano ya FIBA ya Kanda ya Tano kwa timu za vijana chini ya umri wa miaka 16, itakayofanyika Juni, mwaka huu.

 Akizungumza na BINGWA jana, Rais wa TBF, Phares Magesa, alisema Tanzania wanatarajiwa  kuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Magesa alisema wanahitaji udhamini na msaada wa wadau ili kufanikisha maandalizi ya michuano hiyo.

Pia alisema wanahitaji nguvu ya wadau ili waweze kufanyia marekebisho ya Uwanja wa Ndani wa Taifa kabla ya michuano hiyo.

Magesa alisema pamoja na maandalizi mengine, lakini timu zinatakiwa kuanza maandalizi mapema ili ziweza kufanya vizuri.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali wenye mapenzi na mchezo huu kujitokeza na kuzipa nguvu timu hizi ili ziweze kutuwakilisha vyema,” alisema Magesa. Magesa alisema vijana hao wanatarajia kuingia kambini Mei mwaka huu,  Monduli mkoani Arusha .


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*