Tanasha hana mpango wa kujiunga WCB

NA BRIGHITER MASAKI

BAADA ya kuachia ngoma yake ya kwanza inayoitwa Radio, mpenzi wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kujiunga na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Mrembo huyo kutoka Kenya ambaye pia ni mtangazaji wa redio NRG, ameonyesha nia ya kuendelea kufanya muziki mara baada ya wimbo wake huo kupokewa vizuri na mashabiki wa muziki Afrika Mashariki.

“Nadhani aina ya muziki ambayo nafanya ukilinganisha na Wasafi ni tofauti kabisa, labda waanzishe Wasafi Caribbean au Wasafi Hip hop, kitu kama hicho, labda! lakini kwasasa wananisaidia tu kwa kuwasikilizisha nyimbo zangu kabla hazijatoka,” alisema Tanasha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*