TAFF yaomba kuruhusiwa kuendelea na michezo

NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Shirikisho la Soka kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), umeiomba Serikali iwaruhusu kuendelea na michezo yao kwani haina mashabiki wengi sana.

Maombi hayo yamekuja baada ya tamko la Rais Dk. John Magufuli jana, kuruhusu michezo kuendelea kuanzia Juni Mosi, mwaka huu baada ya kuwapo kwa unafuu katika kasi ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya corona.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa TAFF, Mosses Mabula, alisema michezo ya watu wenye ulemavu haina watu wengi sana kama michezo ya watu wasio na ulemavu.

Alisema kuwa mashindano yanayoandaliwa na TAFF, huwa yanawajumuisha wachezaji wenyewe na viongozi, huku mashabiki wakiwa ni wachache mno.

“Tunaomba tuangaliwe kwani hatuna mashabiki wengi sana ambao wanajitokeza kuangalia mashindano yetu,” alisema Mabula.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*