SWAHILI FASHION SASA KWENDA KIMATAIFA

NA JEREMIA ERNEST

MWASISI wa onyesho kongwe la mavazi nchini, Swahili Fashion, Mustapha Hassanali, amezindua rasmi jukwaa hilo litakaloanza Novemba 30 mwaka huu likiwakutanisha wanamitindo wa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo wa Swahili Fashion msimu wa 11, Hassanali alisema mwaka huu tamasha litakuwa na wabunifu wasiopungua 50 kutoka bara lote la Afrika.

“Leo tunazindua msimu huu wa 11 wa Swahili Fashion, tutakuwa na wabunifu wa ndani 30 na 10 kutoka Bara la Afrika huku tukijikita katika kutangaza vivutio vyetu pamoja na Lugha ya Kiswahili,” alisema Hassanali.

Aliongeza kuwa miongoni mwa wabunifu wa mavazi kutoka Bongo watakaopanda kwenye jukwaa hilo ni Martin Kadinda, Kiki Fashion, Afrisolo, Samz na Kitukali kutoka Kenya, Palse wa Afrika Kusini na Afrikawala wa Zambia.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*