SUAREZ AKIRI BARCA INAHITAJI STRAIKA

CATALONIA, Hispania


STRAIKA wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez, amesema ni kawaida kwa klabu yake hiyo kuhusishwa na majina ya washambuliaji mbalimbali, akikiri kwamba wanahitaji nguvu mpya kwenye safu ya mashambulizi.

Suarez alipachika mabao matatu na kuipa Barcelona ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Real Madrid wikiendi iliyopita, lakini anaamini kwamba straika mpya anahitajika ili amsaidie kubeba jukumu la kufunga mabao.

Tetesi za usajili zinaeleza kwamba, huenda Blaugrana wakafanya usajili wa mshambuliaji wa kati kwa ajili ya kumpa changamoto Suarez.

“Barcelona inahitaji namba tisa, kwa umri wangu wa miaka 31 ni kawaida kusikia tetesi hizo kwa sababu klabu lazima ifikirie mbali,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*