Straika KCCA aanika siri za Balinya

NA TIMA SIKILO

STRAIKA wa timu ya KCCA ya Uganda, Allan Okello, ameitaka Yanga kumpa muda Juma Balinya ili waweze kufaidi ubora wake .

Balinya aliyesajiwa na Yanga katika dirisha kubwa la usajili lililofungwa Julai mwaka huu,  akitokea Polisi ya Uganda hajaonyesha ubora wake.

Mshambuliaji huyo alimaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu Uganda, akiwa mfungaji bora aliyefikisha mabao 19.

Akizungumza na BINGWA jana, Okello alisema anamfahamu Balinya ni mchezaji mzuri ambaye alikuwa akiwapa changamoto nchini Uganda

Okello alisema Balinya ni moto wa kuotea mbali japo ameonekana kutokuwa vizuri akiwa ndani ya kikosi cha Yanga.

Alisema anaamini mshambuliaji huyo wa Yanga bado hajaizoea ligi ya Tanzania baada ya  kubadilisha mazingira ambayo inaonakana ni  changamoto kwake.

“Balinya namfahamu sijacheza naye klabu moja lakini ligi yetu ni moja hakuna ambaye hamjui  kutokana na ubora alionao.

“Nadhani mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kwake ametoka Uganda amekuja kucheza Tanzania, akipewa muda wa kutosha watamwelewa ni mchezaji wa aina gani,” alisema Okello.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*