googleAds

Straika avunja mkataba kisa baridi

STOCKHOLM, Sweden

STRAIKA, Musa Noah Kamara, ameamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Trelleborgs kwa madai ya kushindwa kuvumilia hali ya hewa ya baridi iliyopo nchini Sweden.

Uamuzi huo wa Kamara umekuja baada ya mshambuliaji huyo kudumu hapo kwa muda wiki moja tu na klabu hiyo ilithibitisha kuachana na kinda huyo mwenye umri wa miaka 19.

Kamara alisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu ya kuitumikia Trelleborgs, lakini aliamua kuusitisha ghafla, akihitaji kurejea mjini Freetown kwani ameshindwa kuvumilia baridi la Sweden.

Kabla ya kutua Sweden, Kamara alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Sierra Leone mwaka huu baada ya kupachika mabao 15 na kuisaidia timu yake ya East End Lions kutwaa ubingwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*