STERLING AKATAZWA KUTUA ARSENAL

MERSEYSIDE, England

NYOTA Raheem Sterling atakuwa amekiangamiza kiwango chake endapo atakubali kujiunga na Arsenal, kwa mujibu wa mkongwe wa Chelsea, Tony Cascarino.

Sterling raia wa England, amekuwa akihusishwa na dili la kutua Emirates, ikiwa ni sehemu ya ofa ya Manchester City kumpata Alexis Sanchez.

Hata hivyo, straika huyo wa zamani wa Blues, Cascarino, amesema Sterling kutua Arsenal ni kujipoteza, hasa kwakuwa kocha Arsene Wenger ameshindwa kuendeleza wachezaji katika miaka ya hivi karibuni.

“Manchester City wanataka kumwacha Raheem Sterling aende Arsenal, lakini fowadi huyo wa England anapaswa kuogopa kuingia kwenye meli inayozama,” alisema Cascarino.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*