Stars ilale, iamke ifikirie ushindi kwa Wasudan

TIMU ya Tanzania, Taifa Stars, inajiandaa kucheza na Sudan Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salam, ukiwa ni mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani (CHAN), zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon.

Kwa mara ya mwisho Tanzania kufuzu fainali hizo ilikuwa mwaka 2009 zilizofanyika nchini Ivory Coast na sasa inatafuzu nafasi nyingine ya kwenda kucheza fainali za mwakani.

Taifa Stars imeanza vizuri michuano hiyo baada ya kuitoa Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-1, baada ya kutoka sare ya kutofunga mara mbili nyumbani na ugenini.

BINGWA tunaungalia mchezo wa Stars na Sudan, licha ya kuwa itaanzia nyumbani, lakini utakuwa ni mgumu, hivyo hawatakiwi kujiamini kupita kiasi kwani wanatakiwa kusaka ushindi ambao utawaweka katika mazingira ya kusonga mbele watakaporudiana ugenini.

Tunasema kuwa, Taifa Stars wasiidharau Sudan kwa kuwa wenyewe watakuwa kwa lengo la kupata ushindi ili waweze kufuzu michuano hiyo.

Pamoja na Taifa Stars kuundwa na wachezaji wengi wanaochezwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao wanauzoefu mkubwa na michuano ya kimataifa, haitoi nafasi ya kuiona Sudan ni timu inayoweze kufungwa kirahisi.

BINGWA tunasema ili kujihakikishia mapema kufuzu fainali za mwakani wachezaji wa Stars wajue wanajukumu zito la kupata ushindi wa Jumapili, hasa kutokana na rekodi ya hivi karibuni haiko nzuri kwa timu hiyo inapokuwa nyumbani.

Tumeona katika mchezo miwili iliyochezwa hivi karibuni ukiwamo dhidi ya Kenya, Stars ilishindwa kupata matokeo ya ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kutofunga hivyo kuwa na kazi ya ziada ya kupata ushindi ugenini, lakini nao iliambulia matokeo kama hayo na kwenda hatua ya mikwaju ya penalti na kufanikiwa kupita.

Ukiondoa mchezo huo, Taifa Stars ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi katika mchezo  wa marudiano wa kuwania kutinga makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar uliochezwa hivi karibuni Uwanja wa Taifa, lakini ilifanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa matatu 3-0. Kutokana na matokeo hayo, ndiyo maana tunasema kuwa Taifa Stars isijiamini kupita kiasi watapokutana na Sudan, wawe tayari kupata ushindi ndani ya dakika 90.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*