SPURS YAWAWEKEA NGUMU MASHABIKI MAN CITY

 LONDON, England


 

TIMU ya Tottenham Hotspur, inaripotiwa kuweka ngumu kuwalipia gharama mashabiki wa  Manchester City za kwenda kushuhudia mechi yao ijayo ya Ligi Kuu England.

The Lilywhites wamepewa kibali cha kutumia Uwanja wa Wembley kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itapigwa Oktoba  29, mwaka huu, baada ya uwanja wake mpya kushindwa kukamilika kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Man City unataka fidia kwa ajili ya tiketi za mabasi na za  treni ambazo zimeshakatwa na mashabiki kwa ajili ya kwenda kushuhudia mechi hiyo  kama ingepigwa katika uwanja mpya na watoto usafiri wa bure kwa wale ambao watakwenda Wembley.

Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Spurs wamekataa biashara hiyo na huku likieleza kwamba Man City nao wanadai kuwa utata unaofanywa na wenzao hautawasaidia chochote, kwani wataendelea na mipango yao bali walichokuwa wakikitaka ni kuwatendea haki mashabiki wao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*