SPIKA NDUGAI AIPIGA KIJEMBE YANGA

NA RAMADHAN HASSAN,  DODOMA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amepiga vijembe bungeni kuhusiana na matokeo ya mchezo wa Ligi kuu ya Tanzania Bara, kati ya Yanga na Singida United.

Katika mchezo huo, uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni, Spika Ndugai, alisimama na kudai Yanga walifikiri tatizo la timu yao  ni kocha kumbe si kweli.

Spika huyo aliwataka wabunge wawe makini kumsikiliza, huku akimpiga vijembe Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kutokana na matokeo hayo.

Mwigulu anajulikana ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Yanga, lakini pia ni Mkurugenzi wa timu ya Singida United.

“Tusikilizane waheshimiwa, Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mwigulu Nchemba), tusikilizane najua jana Yanga walishindwa kuifunga Singida United tusikilizane kidogo.

“Walifikiri tatizo ni kocha kumbe sio,  ila Yanga wanashida kweli,”alisema huku baadhi ya wabunge wakicheka.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*