Son amzawadia Gomes bao

LONDON, England 

STRAIKA wa Tottenham, Heung-min Son, amemzawadia bao alilofunga dhidi ya Red Star Belgrade kiungo wa Everton, Andre Gomes, aliyevunjika mguu kwenye mechi ya Ligi Kuu England wikendi iliyopita.

Son ndiye aliyemchezea rafu Gomes na kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo huo uliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 lakini Chama cha Soka England (FA) kiliridhia rufaa ya Tottenham na kuifuta kadi hiyo. 

FA iliridhia kuwa Son hakumchezea rafu makusudi Gomes iliyopelekea kuvunjika mguu mbali aligongana naye bahati mbaya katika harakati ya kuwahi mpira.

Katika mechi dhidi ya Red Star Belgrade iliyochezwa ugenini nchini Serbia, Tottenham ilishinda mabao 4-0.

“Namtakia Gomes kupona haraka, haikuwa kusudio langu, nilipata wakati mgumu baada ya ajali ile, nina imani atarudi dimbani na kupona kabisa,” alisema Son.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*