googleAds

Solskjaer: Pogba haendi popote

MANCHESTER, England 

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema kiungo wao, Paul Pogba, hataondoka katika klabu hiyo katika dirisha hili la usajili.

Hofu ilitanda baada ya Pogba kukosa mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya AC Milan juzi, hata hivyo ilithibitishwa kuwa nyota huyo ni mgonjwa.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Solskjaer alisisitiza kuhusu nyota huyo kuwa hatauzwa.

“Nina imani atarudi wiki ijayo, atakuwa tayari kwaajili ya mechi dhidi ya Chelsea. Kumuuza Pogba? Hapana, haendi popote, hilo halina ubishi,” alisema Solskjaer.

Katika matanange huo, Man Uinted iliichapa Milan kwa mikwaju ya penalti 5-4, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Man United tayari imeshakamilisha usajili wa beki wa Leicester City, Harry Maguire, kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 80 (sh bil.223).


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*