googleAds

SINGIDA UNITED WAMNASA KIBOKO WA YANGA

NA WINFRIDA MTOI

KATIKA kuonyesha kwamba imepania kufanya kweli msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida United inamnyatia mkali wa kuibua vipaji anayezitesa Simba na Yanga, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, ili kusaidiana na Hans van Pluijm.

Mexime, ambaye awali alikuwa akihusishwa na mpango wa kutua Yanga kuwa msaidizi wa George Lwandamia, inadaiwa hivi sasa dili hilo linaonekana kufifia na Singida United wameamua kutupa karata yao kwao.

Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu na kocha huyo, zinasema kutokana na kocha huyo kutopenda kufundisha timu kubwa, kuna uwezekano mkubwa akatua kikosi cha United kilichopanda daraja msimu huu.

“Kufanya vizuri kwa Kagera Sugar, ambayo msimu uliopita iliponea chupuchupu kushuka daraja, kumempandisha chati Mexime na kumfanya apokee ofa nyingi. Ila Singida United ina nafasi kubwa kumchukua na wanamtaka na straika wake, Mbaraka Yusuph,” kilisema chanzo hicho.

Kocha Fred Minziro, aliyeipandisha daraja Singida United ambaye awali ilidaiwa ndiye atakayekuwa msaidizi wa Pluijm, bado hajaingia mkataba rasmi na timu hiyo kama alivyolidokeza Bingwa.

“Mimi nipo Dar es Salaam kwa sababu bado tunaendelea na mazungumzo na uongozi wa Singida United kwa mkataba wa kukinoa kikosi hicho Ligi Kuu, kwa kuwa wa awali ilikuwa Ligi Daraja la Kwanza tu,” alisema Minziro.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*