Singida kuonja ladha ya Tigo Fiesta leo

NA MWANDISHI WETU

BAADA ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 kupita na kuacha historia katika miji mbalimbali ya Tanzania, leo hii wakazi wa Mkoa wa Singida nao wanatarajia kuonja ladha ya tamasha hilo litakalofanyika katika Uwanja wa Namfua.

Miongoni mwa vitu ambavyo vinatarajiwa kuongeza ladha ya Tigo Fiesta 2018 ni ubunifu wa wasanii waliopata nafasi ya kutumbuiza, kwani katika mikoa waliyopita kila staa wa muziki aliacha historia kutokana na ubunifu waliokuwa wanafanya kwenye majukwaa kiasi cha kuwapagawisha mashabiki.

Hali kadhalika, Singida leo hii wanatarajia kupata bahati ya kushuhudia ‘vibe’ kama lote kutoka kwa vichwa zaidi ya 16 vya mastaa wa Bongo Fleva, kama vile kundi la Weusi, Fid Q, Chege, Janjaro, Billnas, Rich Mavoko, Lulu Diva, Barnaba, Moni wa Centrozone na kundi la The Mafik.

Wengine ni kundi la Rostam, Jay Melody, Jolie, Benson, Rosa Ree, Whozu na wengine wengi ambao tayari wameshafika Singida kwaajili ya kudondosha vibe kama lote kwa mashabiki zao.

Katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018, Kampuni ya Simu ya Tigo imewaletea promosheni  ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#.

Pia Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Master Pass QR.

Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Master pass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Mpaka sasa tamasha hilo ambalo huwatumia wasanii wa nyumbani kwa asilimia 100, limeifikia miji ya Sumbawanga, Iringa, Songea, Mtwara,Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Msoma, Mwanza, Arusha, Singida, Dodoma, huku kilele chake kikiwa ni Novemba 24 mwaka huu katika uwanja wa Leaders Club, Dar es Salaam.

Msimu wa Tigo Fiesta umeendelea kuacha historia, kwani mbali na burudani, wakazi wa miji hiyo wamekuwa wakifanya biashara mbalimbali zinazowaingizia kipato.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*