SIMBA YATOA KIPIGO KITAKATIFU

NA SALMA MPELI


 

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamezidi kutakata baada ya jana kuishindilia Alliance FC ya Mwanza mabao 5-1 mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara uliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mganda Emmanuel Okwi alipachika mabao mawili dakika tisa na 62, Mghana Asante Kwasi dakika ya 30, Adam Salamba dakika 70 na Clatous Chama dakika 87.

Kwa ushindi huo Simba imepanda mpaka nafasi ya pili ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa huku Azam FC ikiwa na pointi 24 baada ya kuifunga JKT Tanzania.

Alliance FC walianza kwa kasi mchezo huo, ambapo dakika ya sita nusura wapate bao la kuongoza, baada ya Barama Mapinduzi, kuwapangua mabeki wa Simba na kupiga shuti ambalo Manula alijaribu kuokoa, lakini akautema na kumkuta Jamal Mtegeta aliyepiga shuti lililokwenda nje.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*