Simba, Yanga kukipiga Karume Jumapili

LULU RINGO, DAR ES SALAAM

Ligi ya wanawake Tanzania Bara Jumapili Januari 13, itaandika historia ya kwanza toka kuanzishwa kwake, ambapo watani wa jadi Simba Queens na Yanga Princess watachuana.

Yanga Princess ndiye mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ambapo mwenyekiti wa Ligi hiyo, Amina Karuma amesema kila Mtazamaji atakayefika kutazama mtanange huo atatozwa shilingi 2,000.

“Tumeanza ligi kwa kasi kwa sasa tunacheza nyumbani na ugenini hii ni hatua kubwa kwetu, Jumapili Tanzania itaandika historia katika ligi hii, watani wa jadi Simba na Yanga watacheza kuonyeshana nani ni mtemi zaidi, naamini huu utakua mchezo bora na kila mmoja atashuhudia burudani hii kwa shilingi 2,000 tu,” amesema Amina.

Simba Queens inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 10 na Yanga Princess inashika nafasi ya saba ikiwa na alama 6 huku JKT Queens ambaye ni bingwa mtetezi akiongoza ligi hiyo yenye jumla ya timu 12 akiwa na alama 12.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*